Rais JPM, ametangaza kufunga migodi endapo wawekezaji wa migodi ya madini wataendelea kuchelewa kufanya mazungumzo juu ya urejeshaji wa fedha walizozichukua.
Hayo yamezungumzwa katika eneo la Kakonko Kigoma maghiribi mwa Tanzania, na kusema anawasubiri wawekezaji hao waje kwenye mazungumzo, lakini muda ukizidi, mazungumzo hayotokwepo na migodi itafungwa.
Rais Magufuli ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara akiwa kwenye ziara yake ya siku tatu. Amesema haiwezekani makampuni hayo yanaendelea kuwa kimya wakati wameshakubaliana kuanzisha mazungumzo haraka.
“Makampuni ya madini yaliyoahidi kukaa na serikali kuzungumza, wafanye haraka wakiendelea kuchelewa nitafunga migodi yote wanayomiliki” Rais John Pombe Magufuli.
-
Lissu agoma kupima mkojo kwa Mkemia Mkuu, Polisi watoa neno
-
Majaliwa awataka NHC kujenga nyumba katika maeneo mengine ya utawala
Wakati huo huo, Wizara ya Nishati na Madini ya Tanzania imesimamisha shughuli za utoaji leseni za utafutaji na uchimbaji madini, mpaka tume ya madini itakapoundwa na kuanza kufanya kazi rasmi.