Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli leo amemjulia hali mbunifu wa nembo ya taifa aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili pamoja na wagonjwa wengine.

Akiwa katika hospitali hiyo, Rais Dkt. Magufuli amesema kuwa Serikali itaendelea kukabiliana na changamoto zote zinazoikumba hospitali hiyo pia viongozi, madaktari na wauguzi kuboreshewa maslahi yao.

“Madaktari mnafanya kazi nzuri sana, pokeeni pongezi zangu nchi nzima, sisi Serikali tutaendelea kukabiliana na changamoto zinazowakumba mpaka zitakapo malizika, kikubwa ni kumtanguliza mungu mbele mnapofanya kazi ya kuokoa maisha ya watu,” amesema Rais Dkt. Magufuli.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema kuwa tayari madaktari wamegundua magonjwa yanayowasumbua mzee Francis Maige Kanyasu (Ngosha) aliyebuni nembo ya Taifa na mtoto Shukuru Musa aliyekuwa akinywa mafuta na sukari hivyo wanaendelea na matibu vizuri.

Prof. Maghembe atoa neno kwa wavamizi wa misitu.
TRA yawapiga msasa wafanyabiashara wa kichina