Rapa Young Dee aliwaacha watu mdomo wazi baada ya kutamka bila kung’ata ulimi kuwa yeye na muigizaji wa kike Irene Uwoya ni wapenzi!

Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo, Dullah, ndiye aliyepelekea sauti ya Young Dar es Salaam kuwafanya watazamani kushituka na majibu yaliyotolewa, baada ya kumuuliza kuhusu uhusiano wake na Uwoya.

“Ni mpenzi wangu…ndio,” alisema Young Dar es Salaam, kauli iliyomuacha mdomo wazi mtangazaji huyo kwa mshangao mkubwa.

Irene Uwoya na Mwanae

Irene Uwoya na Mwanae

Hata hivyo, rapa huyo aliituliza mshangao wa mtangazaji huyo na ‘attention’ kubwa ya watazamaji aliyoiteka kwa muda kupitia kauli yake, baada ya kueleza kuwa alijibu vile makusudi na kiutani kwa lengo la kuteka umakini wa mtangazaji huyo. Ikumbukwe kuwa Young Dee ana umri mdogo zaidi ukimlinganisha na Uwoya.

“Hapana.. I was just kidding, nilitaka hiyo attention yako,” alisema Young Dee na kueleza kuwa Uwoya ni rafiki yake wa kawaida tu na wamekuwa wakishirikiana katika mambo mengi.

Alimuelezea Uwoya kama mwanamke anayejielewa na mbunge mtarajiwa ambaye amekuwa karibu urafiki wao umekuwa wa karibu kutokana na kazi za sanaa wanazofanya.

Katika kipindi cha hivi karibuni, Young Dee na Uwoya wamekuwa wakipost picha zao kwenye Instagram huku kila mmoja akimpa shavu mwenzake. Hali hiyo ndiyo iliyozua swali la mtangazaji wa kipindi hicho kuhusu uhusiano uliopo kati ya wawili hao.

 

 

 

Magufuli Asema Wagombea Wa Upinzani Ni Chanzo Cha Mgao Wa Umeme
Picha: Lowassa Azidi Kutikisa, Mwanza Yazizima Kumlaki… Aahidi Meli Mpya