Jeshi la kujenga Taifa – JKT, linaendesha zoezi la uchangiaji wa Damu katika maeneo Mbalimbali nchini huku likilenga kukusanya Chupa zipatazo elfu kumi.
Mkuu wa huduma za Sheria Makao Makuu ya JKT, Projest Rutaihwa amesema hatua hiyo ni jitihada za kukabiliana na uhaba wa Damu nchini.
Kanali Rutaihwa ambaye alikuwa akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, amesema takwimu za Wizara ya afya Tanzania ina uhaba wa damu hali inayosababisha wengi kupoteza maisha.
Aidha, amesema JKT ni mdau muhimu kwa jamii hivyo wanakusudia kufanya zoezi hilo kama mfano wa kuigwa huku Hospitali ya Benjamin Mkapa ya Dodoma inakadiriwa kutumia zaidi ya chupa 30 za damu kwa siku wanufaika wakubwa wakiwa wagonjwa wa selimundu.