Mamlaka ya Hali ya hewa TMA imetabiri kuongezeka kwa hali ya joto kali kwa kipindi cha mwezi Novemba na kutegemewa kupungua mwezi Disemba.
Mamlaka hiyo imesema kuwa kipindi hiki cha Joto kinajiri kwa kuwa Jua la utosi limesogea na linatarajiwa kujirudia tena mwezi Februari.
Hadi sasa Mkoa wa Kilimanjaro ambao hutegemewa kuwa na hali ya ubaridi umeripotiwa kuwa na nyuzi joto 36.4 zikiwa zimeongezeka Nyuzi joto 4.6.