Watu 13 wanaaminika wamefariki dunia baada ya mitumbwi miwili waliyokuwa wakisafiria kuzama katika Ziwa Victoria wilayani Bunda mkoa Mara, ambapo jitihada za kutafuta miili zinaendelea.

Inahisiwa kuwa Mitumbwi hiyo ilikuwa imebeba watu 28, tukio hilo walipokuwa wakitoka Kijiji cha Mchigondo kwenda Kitongoji cha Bulomba, kuhudhuria ibada ambapo 14 waliokolewa wakiwa hai na mwili wa mtoto mmoja ulipatikana.

Kati ya Watu waliozama katika ajali hiyo ya majini, 11 ni wanafunzi wa Shule ya Msingi Igundu iliyopo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara, huku ikidaiwa kuwa hali mbaya ya hewa ni moja kati ya sababu zilizokwamisha uokoaji.

Awali, Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Dkt. Vicent Naano alisema, shughuli za uokoaji zilisimama kutokana na hali ya upepo na kwamba walikuwa wakifanya jitihada ili kufanikisha zoezi hilo.

Jengeni hoja acheni kejeli - Kinana
THBUB yataka programu maalum kuwasaidia Wanawake