Hatimaye muigizaji maarufu kutoka nchini Marekani Julia Fox ameamua kuingilia kati tetesi zinazoenea mitandaono kuhusu mahusiano yake na rapa Dizzy Drake, zilizovuma punde baada ya mrembo huyo kuingia kwenye uhusiano wa kimapenzi na Rapa Kanye West ambaye hivi karibuni alimaliza bifu lake na Drake.

Julia ameweka wazi kutofurahishwa na kitendo cha watu kueneza taarifa hizo licha ya kuwa hazina ukweli wowote ndani yake kwa madai ya kuwa Drake alikuwa rafiki yake wa kawaida na hawakuwahi kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kabisa.

Nyota huyo wa Uncut Gems amesema si vyema kushikilia uvumi uliozalishwa kwa lengo la kuharibu ambapo ameutaja mtandao Play Six uliokuwa chanzo cha kwanza cha kuenea kwa uvumi huo.

“Drake ni mtu mzuri na muungwana, Hakuna chochote kilichotokea kati yetu, tulikuwa pamoja kama marafiki wa kawaida tukibarizi.” Alisema Julia Fox

Mrembo huyo aliumwaga ukweli huo Februari 4, 2022, alipokuwa katika Podcast yake na Niki Takesh iitwayo Forbidden Fruits, ambapo ilimlazimu kuizungumzia ripoti ya Page Six iliyodai kuwa yeye na Drake walikuwa na “mapenzi ya siri” kabla ya kuingia kwenye uhusiano na Kanye West.

Ripoti hiyo ilisababisha uvumi mkubwa kote mitandaoni huku kundi kubwa la watu likisubiri kuona ni hatua gani Kanye ataichukua punde baada ya kusikia tetesi hizo.

“Ni wazi niliongea na Kanye kwenye simu siku ya kwanza kabla tetesi hizo hazijaendelea kusambaa zaidi kwa sababu mimi ni mtu muaminifu, nadhani.” Aliongeza Julia Fox.

Maadhimisho ya miaka 45 ya CCM
Kanye West na Kim Kardashian waonesha wazi malumbano kuhusu watoto