Wakati wowote kuanzia leo Jumatano (Septamba 20) Kocha Julian Nagelsmann anatarajia kula shavu kwa kutangazwa kuwa Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Ujerumani akienda kuchukua mikoba ya Hans Flick ambaye alitimuliwa hivi karibuni.

Kwa mujibu wa BILD, Nagelsmann na mabosi wa timu ya taifa ya Ujerumani wapo kwenye hatua za mwisho kwa ajili ya kumpa kazi kocha huyo kijana kukinoa kikosi chao.

Nagelsmann anarejea kwenye soka ikiwa imepita miezi kadhaa tangu alipofukuzwa kazi kwenye kikosi cha Bayem Munich anbapo sababu kubwa ikitajwa kushindwa kutawala kwenye chumba cha kubadilisha nguo (dressing room) cha timu hiyo.

Mara baada ya kutangazwa kuwa kocha wa timu hiyo, Nagelsmann ataanza na mtihani wake wa kwanza wa michuano ya Euro 2024 ambayo itafanyika miezi tisa ijayo huku Ujerumani wakiwa ndiyo waandaaji.

Manyara: Madereva wakutwa na makosa 20,905, wafungiwa
Aubin Kramo kupasuliwa Goti