Aliyewahi kuwa kocha wa klabu za Mwadui FC, Simba SC na Dodoma FC Jamuhuri Kiwelu Julio ameipongeza kampuni ya GSM, kwa kuonyesha uzalendo wa kuisaidia klabu ya Young Africans.

GSM na Young Africans walirejesha vyema mahusiano yao juma lililopita, kufuatia sintofahamu zilizoibuka baina ya pande hizo mbili, na kuibuka taharuki kwa mashabiki na wanachama.

Julio amesema kwa hatua ya uongozi wa kampuni ya GSM ya kukubali kumaliza sintofahamu iliyodumu kwa majuma mawili, imeonyesha dhahir walivyo na mapenzi ya kizalendo na klabu hiyo kongwe hapa nchini.

“Unajua kuchukua timu na kufanya mafanikio kwa faida za watu wengine kama ile Young Africans hakuna tatizo kabisa, ndicho kinachotakiwa endapo inatokea mtu wa aina hiyo na kwa lengo la mafanikio ya timu yenyewe”

“GSM ni mfanyabiashara anafanya vitu kwa faida, lakini kwa mapenzi yake aliamua kuwasaidia zaidi ya mkataba wake na alichowekeza na unajua Young Africans ilikuwa na changamoto nyingi kuanzia usajili, mishahara na mengineyo ya ziada wanapaswa kuungwa mkono na sio kuwabughudhi,”

Hata hivyo Julio amewataka viongozi wa Young Africans kuendelea kuungana na kampuni hiyo katika kuhakikisha wanafanikiwa kufikia mipango waliyokubaliana hususan mfumo wa uendeshaji, ambao utaifanya klabu hiyo kuwa na shindani na sio kuwaacha Simba kuwa na nguvu zaidi.

“Young Africans wakiwa na utaratibu mzuri ikiwemo kuungana na kampuni hiyo wakamilishe mipango yao waliyokubaliana. Naamini kabisa klabu yao ina watu wa maana wanaoweza kufanikisha malengo hayo yatakayowafanya wawe na timu yenye kila kitu na watafurahia ubora walioupoteza.”  Alisema kocha Julio

Clatous Chama ajilipua, aweka hadharani kila kitu
Karia: Hatma ya ligi kuu ipo mikononi mwa serikali