Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 (Ngorongoro Heroes) Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, ametoa sababu za kikosi chake kupoteza mchezo wa kwanza wa Fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Mauritania.

Ngorongoro Heroes ilipoteza mchezo wa kwanza wa ‘Kundi C’ dhidi ya Ghana kwa kufungwa mabao manne kwa sifuri, halia mbayo ilizua minong’ono kwa mashabiki wa soka hapa nchini.

Julio amesema walipoteza mchezo dhidi ya Ghana kutokana na wachezaji wake kushindwa kutumia vizuri nafasi za kufunga, lakini ana matumaini ya kufanya vizuri kwenye michezo ujayo dhidi ya Gambia utakaochezwa kesho Ijumaa (Februari 19).

”Timu ilijitahidi ilicheza vizuri kwani tulitawala mchezo, lakini nafasi tulizozipata hatukuweza kuzitumia vizuri, pamoja na kuwaheshimu Ghana, sio kwamba wametuzidi isipokuwa walipata nafasi na kuzitumia sisi hatukuzitumia vizuri.”

”Tuna amini mechi nyingine tutafanya vizuri hata juzi hatukufanya vibaya sana, nawapongeza wachezaji, ila ugeni wa mashindano ndio uliochangia kupoteza kwa sababu wenzetu wana uzoefu ndio maana wameweza kutumia nafasi walizopata.” Amesema Julio.

Mchezo unaofuta Tanzania itacheza dhidi ya Gambia na mchezo wa mwisho itacheza dhidi ya Morocco Februari 22.

Kocha JKT Tanzania aitangazia vita Polisi Tanzania
Bocco, Mkude kuikosa Biashara United Mara