Aliyekuwa Kocha wa Simba SC na Timu za Taifa za Vijana Jamhuri Kihwelu Julio, ameuvaa Uongozi wa klabu hiyo kwa kusema ulipaswa kumkabidhi majukumu ya Kocha Mkuu Juma Mgunda.
Mgunda alikuwa Kaimu Kocha Mkuu Simba SC baada ya kuondoka kwa Kocha Zoran Maki mwezi Septemba 2022, na alifanikiwa kuifikisha Simba SC Hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.
Julio amesema Uongozi wa Simba SC ulipaswa kuheshimu na kuthamini mchango wa Mgunda alioutoa klabuni hapo, lakini cha kushangaza walimleta Kocha Robertinho, na kumpa jukumu la kuwa Kocha Mkuu, huku kocha huyo mzawa akitangazwa kama Kocha msaidizi.
“Mgunda alistahili kubaki kuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mtu anafanya vizuri na Wachezaji wanamkubali unamtoa kwanini? lakini kwa ‘interest’ za Watu wakaamua kumtoa” amesema Julio alipozungumza na Wasafi FM leo Jumatano (Machi Mosi)