Aliyewahi kuwa Tanzania One ‘Juma Kaseja’ amewashauri Walinda Lango kufanya mazoezi kuliko kushinda mitandaoni kuangalia mazoezi na kwamba kwa sasa nchini kipa wa Young Africans, Djigui Diarra ni bora zaidi.

Msimu uliopita, Diarra ndiye alikuwa Mlinda Lango Bora wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), huku akiisaidia Young Africans kufika fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Kaseja ameyasema hayo kwa kukiri kuwa, kwa sasa Diarra ndiye Mlinda Lango Bora ingawa kuna wengine wakijitoa zaidi wanaweza kufanya vizuri.

“Ubora wake uko juu na mpira wa sasa ni wa kisasa unahitaji kipa anayeweza kucheza kwa miguu na mikono. Ndiyo maana inatoa picha halisi Diarra ana uwezo mkubwa na bora kwa sasa,” amesema Kaseja

Akifafanua juu ya matumizi ya mitandao, kipa huyo mkongwe aliyezichezea timu mbalimbali zikiwamo Simba SC na Young Africans, amesema vijana wengi wa sasa wanaharibiwa na mitandao kwa kufanya mazoezi yanayowekwa mitandaoni na kuona kazi ya ukipa ni nyepesi.

“Utandawazi ni mzuri ila kuna nafasi umewaharibu watú. Kuna vijana wanaamini wakiingia Youtube wakiona wanavyofanya mazoezi makipa wanadhani wanaweza kufanya.

“Kuna wvadogo zetu wanaamini ukifanya vile unaweza kuwa bora, lakini ni kwamba mitandaoni hawawezi kukuwekea kila kitu. Ile ni elimu hawawezi kutoa bure maana nao wanalipia kwa kwenda shule kujifunza. Huko wanaweka vitu vya sekunde tu ambavyo havikufundishi. Rai yangu watoke kwenye mitandao waingie viwanjani wafanye mazoezi,” amesema Kaseja.

Mkataba DP World: Serikali kusimamia maslahi ya nchi
Vita nzito kuibuka usajili wa Harry Kane