Mkurugenzi wa Ufundi wa Simba SC, Juma Mgunda amewataka Mashabiki na Wanachama wa Klabu hiyo kuwa wamoja na kuwapa ushirikiano viongozi wao hasa katika kipindi hiki cha mpito.

Mgunda amesema Simba SC imepita katika kipindi cha mpito na sasa mwanga unaanza kuonekana, ana imani kubwa ya timu hiyo kufikia malengo yao ya kucheza Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kutwaa mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Tanzania Bara ‘ASFC’.

Mgunda amesema kuwa anaifahamu vizuri Simba SC na yaliyopita yalikuwa ni kipindi cha mpito na sasa timu yao imeanza kusimama na kurejea kama ilivyokuwa awali.

Mgunda amesema kuwa Mashabiki na Wanachama wawe na imani na Viongozi, Benchi la Ufundi pamoja na Wachezaji wao kwa sababu ana imani kubwa ya kufanya vizuri katika michezo iliyopo mbele yao hasa mechi zilizosalia za hatua ya Makundi.

“Mashabiki na Wanachama wanatakiwa kusapoti timu yao na kuendeleza kauli mbiu yetu ya Nguvu Moja,” amesema Mgunda.

“Ninaimani na Simba SC, yaliyopita ilikuwa kipindi cha mpito, lakini sasa timu imeanza kurejea katika ubora wake.”

Bosi huyo ameongeza kuwa hana presha kabisa na Kocha Mkuu, Abdelhak Benchikha aliyekuwepo sasa ndani ya kikosi cha Simba SC kwa sababu kuna mabadiliko yameonekana na kuendelea kufanya vizuri.

Kuhusu usajali wa dirisha dogo, Mgunda amewataka Mashabiki na Wanachama kutokuwa na presha muda utakapofika kila kitu kitawekwa wazi na kuona maboresho ya kikosi chao kwa kufuata mapendekezo ya Benchi la Ufundi kulingana na mahitaji ya timu hiyo.

Mafuriko Hanang': Ulega awapa mkono wa pole waathiriwa
Rais FC Barcelona ajitoa muhanga