Aliyekua Kaimu Kocha Mkuu wa Simba SC Juma Ramadhan Mgunda amesema hakuthibitu na wala hatathubutu kuchikizwa na ujio wa Kocha Mkuu Roberto Oliveira Gonçalves do Carmo ‘Robertinho’.

Simba SC ilimtangaza Kocha huyo kutoka nchini Brazil juma lililopita jijini Dar es salaam, kitendo kilimaliza utawala wa Juma Mgunda ambaye alikabidhiwa kazi kuliongoza Benchi la Ufundi, baada ya kuondoka kwa Kocha Zoran Maki, mwezi Septemba 2022.

Akizungumza na Simba TV huko Dubai-Falme za Kiarabu ambako kikosi cha Simba SC kimeweka Kambi Mgunda amesema, amekuwa akiona na kusikia kuwa hakupendezwa na ujio wa kocha huyo na alitamani kuondoka klabuni hapo, kutokana na maamuzi yaliyochukuliwa na Uongozi.

Kocha huyo mzawa amesema bado ni mwenye furaha klabuni hapo na ujio wa Kocha ‘Robertinho’ umekua msaada kwake, kutokana na kujifunza mambo mengi kutoka Bosi huyo ambaye aliiwezesha Vipers SC kutwaa ubingwa wa Uganda msimu uliopita.

“Mimi ninapenda sana kumuamini sana Mwenyezi Mungu kwa kila jambo, pamoja na kwamba tunakwenda vizuri nimeongezewa mtu mwingine, na hili ni jambo jema, kwa sababu lengo la Simba SC ni kufanya vizuri, hivyo kuongeza nguvu hakuna jambo baya.”

“Hii inaonyesha uongozi wa wa Simba SC ulivyokuwa makini na jambo hili, kwa hiyo mimi huwezi kunisikia nikilalamika, zaidi ya kuwasikia watu wakisema kuhusi mimi.”

“Na haiwezekani mimi kuendelea kuunguwa moyoni kwa sababu mimi ndio muhusika, kwa hiyo ninapenda hiki ambacho uongozi umekifanya kwa kutuongezea nguvu katika benchi letu la ufundi.”

“Kwenye mpira jambo hilo halikwepeki, kikubwa ni kwamba huyo aliyeletwa ana levo gani katika ufundishaji wa soka, kwa hiyo kocha yoyote mwenye kutaka kufanya vizuri, kutaka kuendelea kwenye taalum na ukocha unapaswa kujifunza kutoka kwa waliokuzidi.”

“Pamoja na kuwa msaidizi wa Robertinho, pia nipo darasani katika kipindi hiki, ninashukuru sana kwa ushirikiano mkubwa anaonipa na ninamuheshimu kwa sababu amenitambua kama kocha mwenzake.” amesema Mgunda

Atuhumiwa kumuua binti yake kisa Sh 56,000 
Ali Ahamada awajibu wanaombeza