Juma Kassim Nature anaendelea kufanya vizuri hata bila nyimbo mpya huku heshima yake kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Flava, lakini ndoto yake ni kufanya kazi na rapa mkongwe wa Marekani, Snoop Dogg.

Nature amesema kuwa mpango wa kufanya kazi na wasanii wa nje upo na kwamba kuna msanii mmoja wa nje alifanya nae kazi lakini alipoisambaza kazi hiyo haikupata kabisa kuchezwa kwenye vituo vya redio nchini.

“Kazi zinafanyika nzuri, yaani muda wowote wasishangae kazi na Snoop D-o-g-g-y. Wasishangae Snoop Dogg na Msitu wa vina,” Nature aliiambia Planet Bongo ya Channel 5.

Hata hivyo, Nature alisema kuwa kwa sasa anajikita kwanza kufanya collabo na wasanii wa ndani ya nchi kwa sababu bado wasanii wa ndani wanafanya vizuri.

Taarifa Kuhusu Kusimamishwa Kwa Viongozi Wa TEFA
Dk. Ndalichako aagiza NECTA kurudisha mfumo wa 'Division'