Kampuni ya Jumia ambayo imedhamiria kuleta mapinduzi ya biashara kwa njia ya mtandaoni inakuletea Kampeni ya ‘Big Home Makeover’ ambayo inalenga kuwafanya watanzania na wateja wake wote kuwa na nyumba nzuri yenye muonekano wa gharama na kifahari bila kuharibu bajeti zao.
“Amini usiamini, nyumba yako inaweza kuonekana ya gharama na ya kifahari bila kuingia katika madeni. Jibu ni kufanya manunuzi kwa akili”
Uchunguzi wa mtandaoni uliofanywa na Jumia umegundua kuwa asilimia 70 ya nyumba za watanzania hutunza vifaa vyao vya nyumbani kwa muda mrefu bila kujali ubora, upekee wa umri wa vifaa hivyo.
‘’Vifaa vikubwa vya nyumbani kama beseni za kuoshea vyombo, mashine za kupashia chakula, majokofu, na thamani ni vitu vinavyodumu kwa muda mrefu kwa zaidi ya miaka 10.
Jumia wamesema kuwa wamewekeza kwa kiasi kubwa kwa wateja wao, kwani watu huangalia bidhaa zenye nembo kubwa ambazo hudumu kwa muda mrefu. “Inashangaza kugundua kuwa watu hutumia vifaa hivyo kwa muda mrefu! Uchunguzi uanonesha kuwa watu huweka/huhifadhi vitu kwa muda mrefu kadri wawezavyo. Mara nyingi huwa zaidi ya miaka 10 ‘’ amesema Mkurugenzi wa Jumia wauzaji wa vifaa vya nyumbani.
Kampuni hiyo ya Jumia Tanzania imeelewa kuwa kutengeneza/kupendezesha nyumba inaweza kuwa kazi kubwa, na ndio maana wamewaletea watanzania wiki nzima ya kufanya manunuzi ya vifaa vya nyumbani kwa gharama nafuu, kama vile vifaa vya jikoni, sehemu ya kulia chakula, urembo wa nyumbani, beseni za kuoshea vyombo, viosheo na vifutio, jokofu, na jokofu za kugandishia barafu, meza za kupasia nguo, sehemu za kufulia na vitu vingine vingi kuanzia April 16-26.
Jumia wanaendelea kushirikiana na makampuni makubwa yanayoaminika kwa kuuza bidhaa zenye ubora na kwa bei nafuu za vifaa vya nyumbani na kutakuwa na ofa yenye punguzo kubwa la bei.
Bidhaa zinazopatikana ni kutoka makampuni ya Samsung, Bruhm, Nippotec, TCL, Star X, Philips, Aborder, Nikai, Ocean na Tronic, pia kutakuwa na zawadi maalumu wakati tukio linaendelea kama vile kutoa zawadi, kutoa kadi za manunuzi.
Jumia inawawezesha wauzaji kuonyesha na kuuza bidhaa zao moja kwa moja kwa wateja wao, na wateja kuwa na uwanja mpana wa kuchagua bidhaaa kutoka kwa wauzaji wenye bei nafuu zaidi sokoni kwani inatoa suluhisho la bidhaa zote zinazohitajuka na watanzania kwa gharama nafuu, na kukufikishia nyumbani kwako kwa njia rahisi.
Kununua bidhaa kutoka Jumia ni rahisi, peruzi tovuti yao kuchagua bidhaa unayohitaji na uiongeze kwenye kikapu chako mtandaoni kisha hakikisha una acha taarifa zako, na Jumia watakufikishia mpaka mlangoni kwako.
Mkurugenzi huyo wa Jumia ameendelea kuwahamasisha watanzania kutumia fursa hiyo kubwa katika kipindi chote cha kampeni ya ‘Big Home Makeover’ kwani ni kufanya nyumba zao kung’ara bila usumbufu na kwa gharama nafuu.