Siku chache baada ya kutangazwa kuwa meneja wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp ameonyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili kiungo kutoka nchini Ureno na klabu ya FC Porto,  Rúben Diogo da Silva Neves.

Klopp, ameopanga kutimiza dhamira hiyo itakapofika mwezi januari kwa kuamini usajili wa Nevas utaleta tija kubwa kwenye kikosi chake, ambacho kitaaza kupata huduma yake mwishoni mwa juma hili wakati wa mchezo wa ligi kuu ya soka nchini England dhidi ya Tottenham Hotspur.

Nevas, mwenye umri wa miaka 18, amekua katika rada za baadhi ya klabu kubwa barani Ulaya kama Chelsea, Real Madrid pamoja na FC Barcelona na inaaminika kama Liverpool wataingia kikamilifu kumuwania, kutakua na vita kubwa dhidi ya magwiji hao.

Hata hivyo Klopp, ameshaufahamisha uongozi wa Liverpool kuhusu hitaji la kiungo huyo, na amesisitiza jambo la kusajiliwa kwake mwezi januari ili kufikia lengo ambalo linakusuduia huko Anfield.

Thamani na Nevas, inakaridiwa kufikia kiasi cha paund million 29.

Balaa Laendelea Kuikumba Man City
CCM Wajibu, ‘Kama Watakubali Matokeo Iwapo Watashindwa’