Aliyekua meneja wa klabu ya Borussia Dortmund, Jurgen Klopp amekataa kuajiriwa na chama cha soka nchini Mexico, kama kocha mkuu wa timu ya taifa ya nchi hiyo ambayo bado inaendelea kumsaka mbadala wa kudumu wa kocha aliyetimuliwa Miguel Herrera.

Klopp, amekataa kuajiriwa nchini Mexico kwa kuendelea kusisitiza suala la kuhitaji kupumzika kama alivyolitanabaisha mwishoni mwa msimu uliopita wakati alipokua akiagana na viongozi pamoja na wachezaji wa klabu ya Borussia Dortmund.

Katibu mkuu wa chama cha soka nchini Mexico, Guillermo Cantu, amethibitisha kufanyika kwa mazungumzo kati yao na kocha huyo kutoka nchini Ujerumani lakini walipata wakati mgumu wa kufikia lengo lililokua linakusudiwa.

Cantu, amesema jina na Klopp lilipendekezwa katika mkutano wa kamati ya utendaji ya chama cha soka nchini Mexico na kazi ya kumshawishi ili waweze kumuajiri ilianza mara moja, na walifanya mazungumzo na wakala wake mara kadhaa, lakini walikumbana na changamoto kubwa ya msimamo wa kocha huyo.

Mexico, wapo katika mchakato wa kumsaka kocha wa timu yao ya taifa baada ya kumtimua Miguel Herrera, kufuatia kitendo cha utovu wa nidhamu alichokionyesha cha kumpiga muandishi wa habari ambaye aliisema vibaya timu yake wakati wa fainali za kombe la mataifa ya Amerika ya kusini (Copa America) miezi minne iliyopita.

Kwa sasa timu ya taifa ya Mexico inanolewa na kocha wa muda Ricardo Feretti, ambaye ana kazi nyingine ya kukiongoza kikosi cha klabu ya Tigres inayoshiriki ligi ya nchini humo, hali ambayo imekuea ikiendelea kutoa msukumo wa kutafutwa kwa kocha haraka iwezekanavyo.

Mkataba wa Ricardo Feretti, na klabu ya Tigres unatarajia kufikia kikomo mwaka 2017.

Usikose Maajabu Haya Ya Maji…
Baada Ya Ushindi, Mashabiki Wa Simba Wapongezwa