Imefahamika kuwa Meneja wa Magoo wa Jiji ‘Liverpool’ Jurgen Klopp hayupo kwenye kinyang’anyiro cha Kocha Mkuu wa Ujerumani, baada ya hivi karibuni vyombo vya habari vya nchi hiyo kumtaka kuchukua nafasi ya Hansi Flick.

Ujerumani ilipokea kichapo cha mabao 2-0 nyumbani kutoka kwa Colombia mapema juma hili, na kuzua taharuki kwa mashabiki wa Soka nchini humo wakihoji uwezo wa Flick.

Ujerumani sasa wana mechi nne bila ushindi ushindi wao wa mwisho ulikuwa dhidi ya Peru mwezi Machi, huku wakiwa wameshinda mechi tatu pekee kati ya 11 zilizopita.

Kiwango hicho kibaya kinajumuisha mechi za kufuzu kwa hatua ya makundi katika Kombe la Dunia la 2022 kwa mchuano wa pili mfululizo.

Kwa matarajio ya Ujerumani kufanya vyema kama waandaji wa Euro 2024 msimu ujao wa joto, imeweka shinikizo kubwa kwa kocha wa zamani wa Bayern Munich, Flick kubadili mambo.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 aliajiriwa kuchukua nafasi ya bosi wa muda mrefu Joachim Low mnamo 2021 na anaweza kukabiliana na kufutwa kazi bila kuimarika kwa haraka.

Klopp ndiye kocha wa Ujerumani mwenye hadhi ya juu zaidi katika kandanda ya dunia na ndiye anayetajwa sana kupewa kazi hiyo.

Baada ya ombi la wanahabari kwa chama cha soka cha Ujerumani, DFB, kukata Klopp apewe nafasi hiyo, wakala wake amejibu na kusema hawezi kuchukua nafasi hiyo.

“Jurgen ana mkataba wa muda mrefu na Liverpool na DFB ina kocha. Hii sio mada kwetu hata kidogo,” alisema Marc Kosicke wakala wa Klopp akiwaambia waandishi wa habari.

Sagini azindua utawala, usimamizi wa Sheria cha Said Mwema
Afya Tip: Mambo 10 yatakayosaidia uimarishaji Afya ya akili