Bosi wa kikosi cha Liverpool Jurgen Klopp amefungua milango kwa aliyekua nahodha na kiungo wa klabu hiyo Steven Gerrard kurejea Anfield endapo atahitaji.

Klopp ametangaza nafasi kwa Gerrard, baada ya kuona na kusikia gwiji huyo ametangaza kustaafu soka.

Klopp amesema anamkaribisha Gerrard katika benchi la ufundi la klabu hiyo, ili kufanikisha mikakati ya maendeleo ya Liverpool ambayo anaamini anaipenda na kuithamini.

Amesema ni furaha na faraja kufanya kazi na mtu kama Gerrad, kutokana na kutambua mchango wake alioutoa klabuni hapo tangu mwaka 1987 akiwa katika kituo cha kulea na kuendeleza Vipaji kwa vijana cha The Reds.

“Milango ipo wazi kwa ajili yake,” Klopp alisema mbele ya waandishi wa habari.

“Kwa upande wetu hatuna tatizo na suala la Gerrard kurejea hapa, tunamuachia jambo hili ili aweze kufanya maamuzi ya kurejea Anfield ama kuendelea na mipango yake mingine.

“Sina kingine cha kuzungumza, lakini itakua furaha na faraja kwangu na kwa wengine kuona anakubalia kupokea nafasi tuliyompa.”

Gerrard alitangaza kustaafu soka hapo jana, ikiwa ni juma moja baada ya kuamalizana kimkataba na uongozi wa klabu ya LA Galaxy ya nchini Merakani ambayo alianza kuitumikia tangu mwaka 2015.

Alikiba ashinda tuzo mbili za The Nollywood & African Film Critics (NAFCA)
Lionel Messi: FC Barcelona Haitegemei Mtu Mmoja