Meneja wa Majogoo wa Jiji ‘Liverpool’ Jurgen Klopp amesema Mshambuliaji kutoka Uruguay Darwin Nunez ni “mradi wa muda mrefu” klabuni hapo.
Mchezaji huyo wa mwenye umri wa miaka 23, alisajiliwa Liverpool akitokea Benfica ya nchini Ureno kabla ya msimu huu kwa ada ya awali ya pauni milioni 64, amefunga mabao 15 katika michezo 37 msimu wake wa kwanza akiwa na Liverpool, walio nafasi ya nane kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya England na alama tisa kutoka kwenye nafasi nne za juu.
Ingawa, Nunez amepata wakati mgumu wa kucheza katika siku za hivi majuzi, akianza mchezo mmoja tu kati ya nne ya mwisho ya Wekundu hao, huku Klopp akichagua wachezaji watatu mbele, Mohamed Salah, Cody Gakpo na Diogo Jota.
Lakini Meneja huyo kutoka nchini Ujerumani ambaye Jumamosi (april 22) alimkosa Roberto Firmino kwenye mchezo dhidi ya Nottingham Forest kutokana na jeraha la misuli, amesisitiza kuwa Nunez atapata nafasi nyingi ya kucheza katika michezo ya kuelekea mwishoni mwa msimu huu 2022/23.
“Darwin ni mchezaji aliye na ustadi tofauti na wachezaji wetu wengine, ambayo ni nzuri,” alisema Klopp wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kabla ya mechi.”
“Atafunga mabao mengi, na tayari amefunga idadi nzuri. Lakini bila shaka, bado anabadilika. Kiingereza chake bado si kizuri, lakini tunalifanyia kazi hilo.”
“Si muhimu kupitia msimu wa kwanza wakati ni ngumu kwa timu nzima. Mshambuliaji anawezaje kung’aa wakati timu nzima inatatizika? Haiwezekani, lakini amekuwa na wakati mzuri sana.”
“Ninaelewa kwamba anataka kucheza kwa kutamani tangu mwanzo, lakini lazima tutafute njia ambayo inatufanyia kazi tena na kisha inafaa kwa wachezaji ambao tunaweza kuwatumia kwa nguvu maalum.”
“Nina hali sawa kabisa na ninaelewa kuwa Darwin hayuko sawa kila wakati. Hatabasamu usoni mwangu anapogundua kuwa hataanza na kusema: ‘asante, bosi’.”
“Lakini unapokuwa na wachezaji watano au sita mbele, lazima ufanye maamuzi. Mlango uko wazi. Alikuja usiku mwingine na alikuwa wa kipekee. Ilikuwa njia sahihi kabisa. Kwa mechi tano ndani ya wiki mbili zijazo, Darwin ataanza michezo, bila shaka.”