Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amesema katika mchezo wao wa leo Alhamisi (Novemba 30) kwenye michuano ya Europa League dhidi ya LASK Linz, watapambana kuhakilkisha wanashinda na kufuzu hatua inayofuata.

Leo Alhamisi, kuna takribani mechi 16 za Europa League ambapo baadhi ya timu, zitajikatia tiketi ya kufuzu hatua inayofuata ya 16 bora endapo zitaibuka na ushindi, huku zingine zikisubiri hadi mechi zijazo za mwisho hatua ya makundi.

Miongoni mwa timu ambazo ushindi pekee leo zitawafanya wafuzu l6 bora, ni Liverpool ambayo inaongoza Kundi E, itakapokuwa nyumbani kukaribisha LASK Linz kwenye Uwanja wa Anfield.

Liverpool itaingia kwenye mchezo huo ikihitaji pointi tatu pekee ili kufuzu hatua inayofuata, wakati LASK Linz inayoburuza mkia wa kundi hilo na pointi zake tatu, nayo inataka kushinda kufufua matumaini, Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa kuanzia saa 5:00 usiku.

Mechi zingine leo ni; AEK Athens v Brighton, Atalanta v Sporting CP, Maccabi Haifa v Stade Rennais, SC Freiburg v Olympiacos, SK Sturm Graz v Raków, Sparta Prague v Real Betis, TSC Backa v West Ham, BK Hacken v Leverkusen, Marseille v Ajax, Molde v FK Qarabag, Rangers V Aris Limassol, Servette v AS Roma, Sheriff Tiraspol v Slavia Prague, Toulouse v Union St.-Gilloise na Villarreal v Panathinaikos.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 1, 2023
Ancellotti awachimba mkwara waandishi wa habari