Beki kutoka nchini Uholanzi na klabu ya Arsenal, Jurren Timber atafanyivwa upasuaji baada ya kuumia katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu England dhidi ya Nottingham Forest ambao walishinda mabao 2-1.

Beki huyo aliyesajiliwa hivi karibuni kutoka Ajax Amsterdam huenda akawa nje ya dimba msimu mzima na hivyo ni pigo kubwa kwa Mikel Arteta.

Ingawa beki huyo alifanyiwa matibabu akiwa uwanjani na kuendelea na mechi lakini alilizimika kuondolewa baada ya mpumziko. Taarifa ya klabu ikathibitisha ripoti hiyo kupitia akaunti yao: “Baada ya kumfanyia uchunguzi tangu mwishoni mwa juma lililopita baada ya mechi, vipimo vinaonyesha Timber amepata tatizo katika goti lake. Tunathibitisha kwamba kweli amegundulika ana matatizo katika goti”

Pia klabu hiyo ikathibitisha kwamba Mholanzi huyo atafanyiwa upasuaji ili kubaini ukubwa wa tatizo hilo na ikaripotiwa atakuwa nje ya dimba kwa muda wa miezi minane.

Timber alisikitika baada ya kuumia na aliandika ujumbe kupitia akaunti yake ya Instagram: “Nimeumia sana na sikutarajia kama jeraha lingekuwa kubwa zaidi, nilikaribishwa kwa furaha na mashabiki wa Arsenal, nilitaka niwalipe uwanjani lakini haitawezekana kwa sasa, nimebarikiwa kuzungukwa na watu wenye roho ya imani na kwa pamoja tutafanya juu chini ili nirudi uwanjani haraka iwezekanavyo, nitaisapoti timu yangu jukwaani na asanteni kwa kunifanya nijisikie nyumbani na tutaonana.”

Kutokana na kukosekana kwa beki huyo Arsenal inaweza kuongeza kasi ya kutafuta beki mpya atakayeziba pengo au Arteta akampanga Oleksandr Zinchenko mechi zinazofuata za Ligi Kuu ya England ‘EPL’.

Morrison aiwekea mtego Young Africans
NEC yatoa vibali elimu ya mpiga kura uchaguzi mdogo