Wakati dili la beki kisiki wa Ajax na Uholanzi, Jurrien Timber kujiunga na Arsenal dirisha hili likiwa linaenda kukamilika ndani ya juma hili, Mshambuliaji wa zamani wa Ajax na timu ya taifa ya Uholanzi Mark Van Basten amempa onyo kali staa huyu kwa kumwambia anaenda kupotea.

Akizungumza kwenye moja ya vipindi vya Tv nchini Uholanzi, Van Basten alisema Timber amecheza misimu mitatu tu kwenye kikosi cha Ajax na umri wake bado ni mdogo awe makini sana asije kwenda kuwa mchezaji wa akiba kwenye kikosi cha Arsenal.

Usajili wa Timber kwenda Arsenal unatarajiwa kukamilika juma hili na atakuwa England kukamilisha dili hilo la Pauni 45 milioni.

“Ningekuwa mimi ningesubiri kwanza ili nipate uzoefu zaidi, hautakiwi kwenda kujiunga na timu kama sehemu ya timu bali unatakiwa uende kujiunga nayo kama mmoja ya

wachezaji wanaochungwa sana, kila mtu kwenye chumba cha kubadilishia nguo awe anakuangalia na kukutegemea.”

Mkataba wa Timber na Ajax unamalizika mwaka 2025 na tayari ameshafanya makubaliano binafsi na Arsenal na kinachosubiriwa ni waweke pesa mezani kukamilisha mchakato.

Huu utakuwa ni usajili wa pili wa Arsenal baada ya ule wa Kai Havertz aliyesaini dili la miaka mitatu hadi mwaka 2028.

Timber amekuwa akisakwa sana na Manchester United kabla ya dili hilo kufeli dirisha lililopita na ameshawishika na mpango wa Arsenal akiamini atapata nafasi kubwa zaidi ya kucheza akiwa hapo.

Inaelezwa dili hilo kwa asilimia kubwa limesimamiwa na Kocha Mikel Arteta na amekuwa akimshawishi nyota huyo kwa simu mara kwa mara.

Msimu uliopita nyota huyu alicheza mechi 47 za michuano yote na kufunga mabao mawili na kutoa asisti mbili.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Julai 5, 2023
Melis Medo aagiza usajili wa Majimengi