Kocha Mkuu wa Arsenal Mikel Arteta, amepanga kumtumia Jurrien Timber kama beki wa kulia msimu ujao ndani ya kikosi cha Arsenal badala ya beki wa kati.

Arsenal matumaini yao ni kuona wanakamilisha usajili wa beki huyo kutoka Ajax ambapo tayari wamepeleka ofa ya kwanza pauni 30m, lakini kwa bahati mbaya imekataliwa.

Baada ya ofa ya kwanza kukataliwa, Arsenal imepanga kupeleka ofa ya pili kwa Ajax ambao wanahitaji Pauni 50m.

Timber mwenyewe yupo tayari kujiunga na Arsenal licha ya kutakiwa na Mabingwa wa Soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich.

Beki huyo wa kati, tayari amekubaliana na Arsenal ambapo katika dili hilo atakuwa akilipwa pauni 130,000 kwa juma.

Arteta na Mkurugenzi wa Ufundi wa Arsenal Edu, wamefanya makubaliano ya awali na beki huyo ambaye ndani ya Arsenal, wamepanga kumtumia kama beki wa kulia.

Mpaka sasa, Arsenal imekamilisha dili la Kai Havertz kutoka Chelsea, huku ikiendelea kupambania saini ya Timber na Declan Rice.

Valverde awekwa sokoni kwa Milioni 90
Sadio Kanoute mambo safi Simba SC