Justin Bieber amepata shukurani nyingi kutoka kwa mashabiki wake kutokana na tendo jema alilolifanya baada ya kumuona mwanamke wa makamo aliyekuwa akilia barabarani baada ya kupata ajali ya gari.

TMZ imeripoti kuwa tukio hilo lilitokea Jumatano majira ya usiku ambapo Bieber na marafiki zake walikuwa wanatoka kula bata kwenye kumbi za starehe na kabla ya kufika katika eneo hilo.

Polisi wameueleza mtandao huo kuwa mwimbaji huyo na rafiki zake walisimamisha gari na kujaribu kumpa msaada mwanamke huyo aliyekuwa anapiga kelele za kuomba msaada. Wakati Bieber akishughulika na mwanamke huyo aliyedaiwa kugongwa na gari na mtu aliyekimbia baada ya tukio hilo, wapambe wa mwimbaji huyo walipiga simu kuita polisi.

Bieber Gari

Hata hivyo, baada ya Polisi kufika katika eneo la tukio, mwanamke huyo alikataa kupaga ambulance huku akieleza kuwa hakuumia sana na alianguka chini tu kidogo. Lakini mashuhuda wanaeleza kuwa gari lenye rangi nyeusi liliondoka haraka baada ya kusababisha ajali hiyo.

 

Clinton kumteua Obama kuwa Jaji wa Mahakama Kuu
Makaburi ya raia ya pamoja ya mamia yagundulika Burundi

Comments

comments