Mwimbaji Justine Bieber amelipiga teke ‘gunia la pesa’aliloahidiwa kupewa kwa kushiriki katika filamu iliyotabiriwa kuwa kubwa kutoka Hollywood, baada ya kupewa nafasi ya kuigiza kama mtu anayeshiriki mapenzi ya jinsi moja (shoga).

Kwa mujibu wa New York Post, Bieber alitakiwa kuigiza kwenye filamu ya ‘Uber Girl’ kama kijana mdogo maarufu anayefanya muziki wa pop, lakini mwenye tabia za ushoga na alitakiwa kuoneshwa akiiigiza scene inayomuonesha akifanya mapenzi.

“Amekataa kabisa kushiriki hadi waondoe kabisa wazo la kumhusisha na kufanya mapenzi ya jinsia moja na mwanaume mwenzake ambaye anatakiwa kuonekana kama ni mmoja kati ya ‘dancers’ wake,” mwandishi Pete O’Neill aliiambia New York Post.

Justin Bieber 2

Mashabiki wengi wamempongeza Bieber kwa uamuzi huo wakidai kuwa umeonesha ni jinsi gani kweli amekuwa mkubwa hata kiakili.

Francis Coquelin Kuziba Nafasi Ya Per Mertesacker
Saa 48 Zijazo Kuamua Hatma Ya Paul Pogba