Mwimbaji kutoka Toronto nchini Canada, Justin Bieber anadaiwa kuanza kwa vitendo safari yake ya kumrudia Mungu aliyokuwa akiizungumzia mara kwa mara, baada ya kuahirisha ziara yake.
Mtangazaji wa kituo cha runinga cha ‘Channel Nine’, Richard Wilkins amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa mtu wa karibu wa Bieber kuwa kuahirisha ziara hiyo ni hatua yake ya kutaka kujikita zaidi kwenye masuala ya kiimani ikiwezekana kuanzisha kanisa lake.
“Ninalazimika kuamini kuwa sababu halisi ya kuachana na ziara yake ni kutaka kuirudia zaidi imani yake na anaweza hata akawa na mpango wa kuanzisha kanisa lake mwenyewe,” Richard alifunguka.
Bieber ambayee alilelewa katika familia iliyokuwa ikishikilia imani ya dini ya kilokole ambapo mama yake mzazi alikuwa muumini wa dhehebu moja la kilokole (born again), amekuwa akieleza mara kadhaa kuwa anasikia wito wa kumrudia Yesu.
- Marekani kuweka vikwazo dhidi ya maadui zake
- Exclusive: Vanessa afunguka anachofanya akipigwa na misukosuko, stress (Video)
Mkali huyo wa ‘What Do You Mean’ amewahi kukaririwa akisema kuwa kila siku anasikia wito zaidi ya jana wa kuirudia imani yake.
Hata hivyo, kuna taarifa kuwa huenda Bieber ameamua kuahirisha ziara hiyo ili aweze kupumzisha koo lake kutokana na matatizo ya kiafya yanayowapata wasanii wengi kwa kufanya matamasha mengi bila kupumzika.
Mwimbaji John Mayer ambaye ni mtu wa karibu wa Bieber amekaririwa na E-News kwenye ukurasa wao wa Instagram akieleza kuwa endapo angeendelea na ziara hiyo huenda angejiumiza kama walivyofanya wasanii wengi wakubwa ambao amedai wamepotea kutokana na tatizo hilo.