Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Ajax Amsterdam Justin Kluivert, leo anatarajiwa kufanyiwa vipimo afya mjini Roma, ikiwa ni sehemu ya kukamilisha usajili wake ndani ya klabu ya AS Roma inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Italia Serie A.

Justin ambaye ni mtoto wa nguli za zamani wa timu ya taifa ya Uholanzi Patrick Kluivert jana jioni aliwasili mjini Roma, baada ya kukamilika kwa mazungumzo kati ya viongozi wa klabu za Ajax Amsterdam na AS Roma.

AS Roma walithibitisha kuwasili kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 kupitia tovuti ya klabu yao http://www.asroma.com/en/news/2018/6/justin-kluivert-arrives-in-rome along with a picture of Kluivert’s arrival.

Msimu uliopita Justin Kluivert alifanikiwa kufunga mabao 10 katika michezo 30 ya ligi aliyocheza, na kwa mara ya kwanza aliitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uholanzi mwezi Machi.

Ada ya uhamisho wa Justin inatajwa kufikia Euro milioni 20, sawa na dola za kimarekani milioni 23.51.

Daruso: Taarifa kuhusu marehemu kufariki na ujauzito zipuuzwe
Video: Young Dee aahidi makubwa ''Hatutaki kufunikwa''