Klabu ya Juventus ni kama imeanza kurejea katika makali yake kwani mpaka sasa wapo ndani ya michuano mitatu tofauti ingawa ndoto ya ubingwa Serie A kwao haipo.

Timu hiyo kwa sasa ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa Serie A ikiwa chini ya Kocha Allegri, ikivuna alama 59, baada ya michezo 31, ikishinda michezo 18 na kupoteza nane ndani ya Serie A.

Klabu hiyo licha ya kupitia kipindi kigumu, ipo katika Nusu Fainali ya Europa League na itacheza dhidi ya Sevilla ambao wana historia na taji hilo.

Juventus wapo pia katika michuano ya Coppa Italia ambako wametinga hatua ya Nusu Fainali.

Hapa unaona namna gani Allegri alivyoipambania timu yake hiyo kurejea katika mstari licha ya msimu huu kuwa na majeruhi wengi ambao walikaa nje kwa muda mrefu.

Uongozi Simba SC wasisitiza rekodi Afrika
Young Africans yazidisha jeuri Afrika