Mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC, wameripotiwa kutuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji kutoka nchini Chile na klabu ya Arsenal, Alexis Sanchez.

Baadhi ya vyombo vya habari nchini Italia, vimeripoti kwamba, Juventus wamewasilisha ofa hiyo ya Pauni milioni 25.7 ambazo ni sawa na Euro milioni 30, huko kaskazini mwa jijini London yalipo makao makuu ya klabu ya Arsenal.

Kwa muda wa majuma kadhaa, Juventus wanatajwa kuwa katika harakati za kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27, ambaye alisajiliwa na The Gunners miaka miwili iliyopita akitokea FC Barcelona.

Taarifa zaidi zinaeleza kwamba, Sanchez ameshaonyesha nia ya kutaka kuondoka Etihad Stadium katika kipindi hiki cha majira ya kiangazi, lakini uongozi wa Arsenal unatilia mkazo suala hilo kufanyika.

Sanchez ameshawahi kuishi na kucheza soka nchini Italia kwa muda wa miaka mitano kuanzia mwaka 2006 hadi 2011, akiwa na klabu ya Udinese  na baadae alitimkia nchini Hispania kujiunga na klabu ya FC Barcelona.

Chelsea Wajitosa Kwa Kalidou Koulibaly
Jerry Muro: Nitakaa Kimya Kama Yanga Wataninyamazisha