Wachezaji wa wote wa klabu ya Juventus wamelazimika kujitenga kwa ridhaa yao baada ya kiungo wa timu hiyo Weston McKennie kuthibitika kuwa na virusi vya Corona.

Weston McKennie ambaye amejiunga na Juventus katika dirisha hili la usajili akitokea Schalke ya Ujerumani, ndio mchezaji pekee wa Juventus kuthibitika kuwa na maambukizi hayo kati ya wachezaji wote hivyo wanajitenga kwa tahadhari.

Taarifa hizo zinakuja ikiwa ni saa 24 zimepita toka Cristiano Ronaldo wa Juventus athibitike pia kuwa na maambukizi ya Corona akiwa kwao Ureno  na sasa amejitenga.

Azam FC: Tupo kamili kuikabili Mwadui FC
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Oktoba 15, 2020