Klabu ya Juventus iko mbioni kutaka kumsajili mchezaji wa Manchester United, Jadon Sancho katika kipindi cha dirisha dogo la usajili la mwezi Januari 2024, kwa mujibu wa ripoti.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka alizuiwa kufanya kazi katika shule ya soka baada ya kuzozana na Ten Hag baada ya kumkosoa hadharáni sababu za kumtema mchezaji huyo katika kikosi cha Arsenal mwezi uliopita, bado hajamuomba radhi Ten Hag kama alivyokata kocha huyo wa Man United, ambaye alisema kuwa mchezaji huyo hayuko katika mipango yake.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun, Juventus wako tayari kumsajili Sancho, lakini kwa sharti la kumchukua kwa mkopo ikiwa United watakubali kumlipa nusu ya mshahara wake wa Pauni 350,000 (sawa na Sh bilioni 1) kwa juma.

Vigogo hao wa ltalia wako tayari kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa England kwa mkataba wa kudumu katika kipindi kijacho cha majira ya joto kwa ada ya Pauni milioni 60 (sawa na Sh bilioni 183).

Sancho alitolewa katika mazoezi ya Man United baada ya kulalamika katika mitamdao ya kijamii kuwa alifanywa mbuzi wa kafara na kudaiwa kumuita Ten Hag muongo baada ya timu yao kufungwa na Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Sancho, aliyejiunga akitokea Borussia Dortmund mwaka 2021, ameichezea United mara tatu akitokea benchi msimu huu, lakini hajaichezea klabu hiyo tangu mzozo huo ulipoibuka.

Winga huyo alifunga mabao 12 na kusaidia kupatikana kwa mabao sita kutoka katika mechi 82 alizocheza, na kuweka hatima yake kuwa matatani katika klabu hiyo kuelekea dirisha la usajili la mwezi Januari 2024.

Kutokuwepo kwake, kumeifanya Man United kutofanya vizuri katika michezo dhidi ya Brighton, Bayern Munich, Crystal Palace na Galatasaray tangu mchezaji huyo atoke katika klabu hiyo.

Lakini Mashetani hao Wekundi walirudi katika ushindi pale walipocheza dhidi ya Brentford juzi Jumamosi (Oktoba 07), shukrani kwa bao la muda wa majeruhi la Scott McTominay.

TPBRC: Ni zamu ya mabondia Wanawake
Maafisa Al Ahly watua Dar kimya kimya