Klabu ya Juventus inafikiria kuvunja mkataba wa kiungo Paul Pogba wenye thamani ya Pauni l30,000 kwa juma baada ya kufungiwa kutokana na kufeli vipimo vya dawa za kuongeza nguvu michezoni.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 30, amepigwa ‘stop’ kwa muda usiojulikana na huenda akatúmikia adhabu hiyo kwa muda wa miaka minne.
Ripoti ya vipimo vyake vilitolewa baada ya mechi ya Serie A dhidi ya Udinese tangu Agosti 20 hata hivyo kiungo huyo hakucheza.
Shirika la kuzuia dawa za kuongeza nguvu Italia limemsimamisha, Pogba na ana siku chache za kutuma vipimo vingine ‘Sample B’.
Sheria ya adhabu matumizi ya dawa za kuongeza nguvu kwa kesi kama hiyo ni kifungo cha miaka minne au miwili kama ikigundulika alitumia bila kukusudia.
Kutokana na hilo Juventus inafikiria kuvunja mkataba wake na kiungo huyo.
Pogba alisaini mkataba wa miaka minne aliporejea akitokea Manchester United mwaka jana, hiyo inamaanisha ámebakiza mkataba wa miaka mitatu kukipiga Juventus.
Aliporejea Turin, taarifa ziliripoti Pogba alikubali kukatwa mshahara kutoka Pauni 290,000 hadi Pauni 130,000 kwa juma.
Aidha wakala wa Pogba, Rafaela Pimenta, alimtetea Pogba akisema: Tunasubiri mpaka ishu yake itakapojadiliwa hatutazungumza kitu kwa sasa.”