Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus wamepewa ruhusa ya kuzungumza na kiungo kutoka nchini Ujerumani, Julian Draxler, ili kukamilisha sehemu ya usajili wake wa mkopo.

Schalke 04 wanaommiliki kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21, wametoa ruhusa hiyo kwa kuamini kuna nafasi nzuri kwa viongozi wa klabu ya Juventus kumalizana na Draxler ili kupisha mambo mengine ya usajili wake kuchukua nafasi.

Mkurugenzi wa michezo wa klabu ya Schalke 04, Horst Heldt, amesema Juventus walionyesha nia ya dhati ya kutaka kumsajili Draxler kupitia wakala wake, lakini waliona hakuna umuhimu wa kumuachia moja kwa moja moja na badala yake wameamua kumtoa kwa mkopo.

Hata hivyo, kuna tetesi zinazoendelea katika baadhi ya vyombo vya habari nchini Italia pamoja na Ujerumani, zikidai kwamba huenda Draxler, akaingia katika ushawishi wa kusajiliwa moja kwa moja kwa mabingwa hao wa Sirie A, baada ya kumaliza mkataba wake wa mkopo endapo ataonyesha kiwango kitakachowavutia viongozi Juventus.

Msimu uliopita Draxler alitamani kuondoka nchini Ujerumani na kuelekea sehemu nyingine barani Ulaya kucheza soka lake, lakini kizingiti cha safari yake kilikua ni ada ya usajili ambayo ilifikia paund milion 35.

Uongozi wa klabu ya Schalke 04, umekua ukiamini kiungo huyo ana thamani kubwa kutokana na kiwango pamoja na umri mdogo alionao, na amekua muhimili muhimu kwenye kikosi chao kilicho na maskani yake makuu hukoVeltins-Arena, Gelsenkirchen.

Patrick Bamford Akamilisha Usajili Crystal Palace
Mrisho Mpoto Ahofia Upepo Wa ‘Timu Fulani’ Kumkosesha Ushindi AFRIMMA