Mkurugenzi mkuu wa klabu bingwa nchini Italia Juventus, Giuseppe Marotta, ametangaza kusitisha mpango wa usajili wa kiungo kutoka nchini Brazil pamoja na klabu ya Chelsea, Oscar dos Santos Emboaba Junior.

Marotta, ametangaza kusitisha mpango huo, huku vyombo vya habari vikiwa vimesha waaminisha wadau wa soka barani Ulaya juu ya uhakika wa kusajili kwa kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23.

Oscar alikuwa anapewa nafasi kubwa ya kusajiliwa huko mjini Turin baada ya kuondoka kwa kiungo kutoka nchini Chile, Arturo Vidal, ambaye ameelekea nchini Ujerumani kujiunga na klabu bingwa nchini humo FC Bayern Munich.

Marotta amesema kusitishwa kwa mpango wa usajili wa kiungo huyo, kumetokana na mikakati mipya ambayo imewasilihwa kwake na kitengo cha ufundi ambacho kimesisitiza kuhitaji kiungo mwenye sifa tofauti na Oscar.

Hata hivyo, Juventus walikuwa wameshaanza kuhusishwa na tetesi za kumsajili kiungo kutoka nchini Hispania na klabu ya Real Madrid, Francisco Román Alarcón Suárez Isco, lakini bado wamekanusha kuwepo katika mpango huo.
Kufuatia hali hiyo bado haijafahamika ni wapi Juventus watakapopeleka mashambulizi ya kumsaka mbadala wa Arturo Vidal.

Kwa sasa Juventus ina viungo wenye hadhi kubwa duniani kama

Paul Pogba, Claudio Marchisio, Sami Khedira pamoja Roberto Pereyra.

Hali Tete Kwa Mulumbu, Aanza Vibaya Norwich City
Chadema wawakabidhi Jahazi Lowassa na Juma Duni, wabadili jina la ‘Safari ya Matumaini’