Mabingwa wa soka nchini Italia, Juventus wanaongoza kuwa na wachezaji wengi katika orodha iliyotolewa na shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, kwa ajili ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa barani humo.

Juventus ambao msimu uliopita walitinga katika hatua ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya na kutandikwa mabao matatu kwa moja dhidi ya FC Barcelona, wamepata bahati ya kuwa na wachezaji watano katika orodha hiyo.

Gigi Buffon, Paul Pogba, Arturo Vidal, Carlos Tevez pamoja na Andrea Pirlo ni wachezaji kutoka kwenye klabu hiyo ya mjini Turine ambao watashindana na Leo Messi, Andres Iniesta pamoja na Neymar kutoka FC Barcelona, Cristiano Ronaldo wa Real Madrid pamoja na Eden Hazard Chelsea.

Orodha hiyo imetolewa na UEFA baada kazi nzuri ya mchujo iliyofanywa na jopo la ufundi la shirikisho hilo kwa kusaidiana na waandishi wa habari ambapo mchujo umefanyika kutoka wachezaji 54 hadi kufikia 10.

Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa barani Ulaya, anatarajiwa kutangazwa katika hafla maalum iliyopangwa kufanyika nchini Ufaransa August 28.

Forbes: Real Madrid Bado Tishio Kwa Utajiri Duniani
Mchezaji Mtanzania Mwingine Apata Dili Ujerumani