Msanii wa RnB Bongo, Juma Jux ambaye kwa sasa anafanya vizuri na kibao chake kinachoenda kwa jina la utaniua, mapema leo hii ametoa sababu iliyomfanya kwa miaka mingi asifanye sherehe yake ya kuzaaliwa maarufu kama ‘Birthday Party’ hivyo kesho anatarajia kuifanya na kusherekea siku hiyo na mashabiki zake.

Kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika waraka ambao ndani yake amemzungumzia Vanessa Mdee kuwa ndiye chanzo kilichomfanya asiifikirie sherehe hiyo, na kusema kuwa kwa kipindi hiko ndiye aliyekuwa mpenzi wake rafiki yake na mtu wa karibu sana.

Hivyo hakuwa na sababu ya kufanya sherehe hiyo kama ilivyo kwa watu wengine.

Jux amesema kuwa uwepo wa aliyekuwa mpenzi wake Vanessa Mdee  ulikuwa ni zaidi ya kitu chochote  kwenye siku yake ya kuzaliwa na anasikitika kuwa kwa sasa wamebaki kama marafiki wa kawaida.

” Kuongea na yeye au text yake tu ilitosha kukamilisha siku yangu, ila sasa sidhani kama itakuwa kama mwanzo, nitafarijika sana kama  nikimuona hiyo siku”. amesema Jux.

Ameeleza kuwa mara yake ya mwisho kufanya sherehe hiyo ilikuwa 2013 miaka minne iliyopita, hivyo kwa mwaka huu amesema anataka kusherekea na mashabiki wake.

Aadhibiwa kwa kusambaza tetesi za mke wa Rais kuolewa na Dr. Dre
Diego Costa kusajiliwa kwa mkopo Hispania