Jux ametangaza kutoa zawadi kwa shabiki yake atakayeweza kubashiri siku na muda atakaoachia wimbo wake mpya ‘I love you’ alioshirikiana na nyota kutoka nchini Ghana Gyakie.

Kupitia kwenye ukurasa wa mtandao wa Instagram Jux amesema kuwa atatoa zawadi ya shilingi Laki moja ikiwa atajitokeza shabiki atakayepatia chemsha bongo hiyo.

“My amazing fans, Wiki ijayo nina jambo lenu nalileta mjini. Tanzania X Ghana, Video yangu ya wimbo wangu na Gyakie I LoveYou iko tayari, Itatoka wiki ijayo, Ninachohitaji kutoka kwako ni kuniambia hiyo video nitaitoa lini na saa ngapi?.

Ukipatia siku husika na saa ya kutoka video ya #ILoveYou utafurahia, nina zawadi yako ndogo ya Shillingi Laki moja, let’s get busy my people.” Ameandika.

Baraza kuu la Umoja wa mataifa kujadili Ukraine kwa dharura leo
Watalii kutoka Ukraine wakwama Zanzibar