Mkuu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Jenerali Venance Mabeyo amewasamehe vijana 853 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kuandamana kwenda Ikulu wakishinikiza kuajiriwa jeshini.

Aidha Aprili 17, 2021 Jenerali Mabeyo akiwa katika hafla ya kuwatunuku kamisheni maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mjini Dodoma, alitangaza kuwafukuza vijana 854 ambao mmoja amefariki kwa kukiuka taratibu za jeshi kwa kuanzisha mgomo Aprili 8, 2021 na kufanya maandamano kwenda Ikulu ya Chamwino Dodoma, kwa madai ya kutaka kumuona Rais ili wadai kuandikishwa jeshini kama walivyoahidiwa na aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Machi 5, 2022 msemaji Mkuu wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Luteni Kanali Gaudentius Ilonda amesema Jenerali Mabeyo ametoa msamaha kwa vijana hao na kuwataka kurejea kwenye makambi kwaajili ya kuendelea na mafunzo mara moja.

Amesema kuwa kabla ya msamaha huo, JWTZ lilifanya uchunguzi na utafiti wa kina mkoa kwa mkoa, wilaya kwa wilaya, kata kwa kata na kijiji kwa kijiji na kujiridhisha kuwa vijana hao walishawishiwa kwa mambo mbalimbali ikiwemo utoto na kutokujitambua, lakini pia kutokokujitambua na baadhi kurubuniwa.

Vijana wote 853 wanatakiwa kupokelewa ifikapo Machi 12,mwaka huu katika kambi 841 JKT iliyopo Mafinga mkoa wa Iringa.

Hali kadhalika ametoa wito kwa wale wenye vitendo vya kuwarubuni vijana walioko kwenye kambi zao, kuacha mara moja kwani Jeshi liko imara katika kulinda mipaka ya nchi, Katiba pamoja na kumtii Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Urusi yasitisha mapigano Ukraine

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Machi 6, 2022
Ashindwa kuondoka Ukraine baada ya kubadili Jinsia