Afisa mtendaji mkuu wa Namungo FC Omar Kaaya na Wachezaji Lukas Kikoti pamoja na Hamis Fakhi wanatarajiwa kuwasili nchini leo Jumanne (Machi 02), wakitokea Angola walipokuwa amewekwa ‘Karantini’ kwa siku kadhaa.

Kiongozi Kaaya na wachezaji hao wawili walianza safari jana kupitia Ethiopia, huku wakimuacha mchezaji Fred Tangalu ambaye bado vipimo vyake havijatoka.

Juma lililopita ilithibitika kuwa wachezaji na kiongozi wa Namungo FC waliruhusiwa kutoka Karantini, lakini taarifa za Tangalu zimeibuka siku chache kabla ya kuanza safari ya kurejea nchini.

Wachezaji na kiongozi huyo walikwama wakati walipokwenda mjini Luanda kwa ajili ya mchezo wa hatua ya 32 Bora ya Kombe la Shirikisho dhidi ya 1 de Agosto pamoja na mwingine Fred Tangalo ambaye amebaki Angola.

Hata hivyo Shirikisho la Soka Barani Afrika ‘CAF’ liliamuru michezo miwili ya hatua hiyo kwa timu hizo kuchezwa jijini Dar es salaam, ambapo Namungo FC waliibuka na ushindi wa jumla wa mabao saba kwa matano na kutinga hatua ya makundi.

Namungo FC imepangwa kundi D sanjari na klabu za Raja CA (Morocco), Pyramids FC (Misri)  na Nkana FC (Zambia).

Simba SC kuifuata Al Merrikh
Prof. Kabudi apokea nakala za hati za utambulisho za Mabalozi wateule