Wakili Mwandamizi wa Serikali, Wankyo Simon ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa upelelezi wa kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili Mwandishi wa Kujitegemea wa Habari za uchunguzi, Erick Kabendera bado haujakamilika

Kabendera anashtakiwa kwa Makosa matatu ikiwemo kukwepa Kodi kiasi cha Tsh. Milioni 173,247,047.02, Utakatishaji Fedha na kujihusisha na genge la uhalifu Makosa ambayo yote hayana dhamana

Aidha, Kabla ya kushtakiwa kwa Makosa tajwa hapo juu, Kabendera alihojiwa na Jeshi la Polisi kwa kuwa na mashaka juu ya uraia wake na baadaye kudaiwa kukiuka sheria ya Makosa mtandaoni (Cyber Crimes Act) hadi aliposomewa mashitaka ya uhujumu uchumi.

Hata hivyo, mwandishi huyo wa kujitegemea ambaye amekuwa akichapisha habari zake katika vyombo mbalimbali nchini na ulimwenguni alikamatwa nyumbani kwake Mbweni jijini Dar es salaam, mnamo Julai 29, 2019.

Rais wa Chad atangaza hali ya dharura
RPC Shana atoa angalizo, ' Wazazi tunzeni silaha zenu vizuri'