Kesi inayo mkabili Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva pamoja na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu, imetajwa tena hii Leo katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar esaalaam.
Jopo la mawakili wa upande wa jamuhuri likiongozwa na Leonard Swai wameomba kusogezwa mbele tarehe ya kusikilizwa kesi hiyo kutokana na upelelezi kutokamilika.
Hata hivyo kwa upande wa utetezi ukiongozwa na Mutakyamirwa Phelemon pamoja na Evodias Mtawala wameomba kuharakishwa kusikilizwa kwa kesi hiyo.
Aveva na kaburu walifikishwa mahakamani hapo Julai 3 mwaka huu na kusomewa mashtaka 5 yakiwemo ya kujilipa madeni ya kiasi cha dola 300,000 na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (takukuru).
Kesi hiyo imeahirishwa hadi August 16 mwaka huu na watuhumiwa wamerudishwa tena rumande hadi tarehe ya kusikilizwa kwa kesi hiyo.