Askofu mkuu mjini Kigali Antoine Kambanda, ameweka historia kwa kuwa Kadinali wa kwanza nchini Rwanda kuwa miongoni mwa makadinali wapya waliotajwa na Papa Francis jana Jumapili kufika nafasi ya juu ya uongozi katika Kanisa Katoliki.

Baada ya tangazo la Papa, Askofu Mkuu Kambanda ameiambia televisheni ya taifa ya Rwanda kuwa “hiki ni kitu ambacho hata sikuwahi kufikiria kwamba kinaweza kutokea”.

Askofu mkuu Kambanda ndio Kadinali pekee wa Afrika aliyetajwa miongoni mwa makadinali 13, ambao watatawazwa katika sherehe itakayofanyika Vatican Novemba 28.

Rwanda, nchi yenye idadi kubwa ya waumini wa Kikatoliki inaungana na Kenya, Uganda na Tanzania, kama nchi za Afrika Mashariki kuwa na makadinali hivi karibuni.

Kati ya idadi ya Makadinali 219 kote duniani sasa hivi, 29 pekee ndio wanaotoka Afrika.

NEC yakanusha madai uwepo wa vituo hewa vya wapiga kura
Masau Bwire: Simba SC watakutana na mpira KAUKAU