Mkali wa mitindo na mbunifu wa mavazi, ambaye pia ndiye msimamizi wa kazi za Tz sweetheart yaani Wema Sepetu hapa Tanzania Martin Kadinda ameeleza magumu, changamoto na udhaifu wa mlimbwende huyo pindi wanapokuwa kazini na hata katika maisha nje ya kazi.

Kadinda ameeleza kuwa pamoja na Wema Sepetu kufanya kazi zake zinazoonekana na kupendwa na mashabiki wake ameeleza kuwa msanii huyo wa maigizo anatatizo moja la kutobadilika kitabia.

”Licha ya Wema Sepetu kuwa mtu muhimu kwenye maisha na kazi zake, amekuwa mtu ambaye habadiliki” amesema Martin Kadinda.

Kutokana na tabia hiyo Martin amesema kuwa inamuwia vigumu kumtengenezea mazingira mazuri ya kazi zake kwa maisha yake ya sasa na baadae ili aweze kuheshimika.

Amesema changamoto kubwa kwa Wema ni kwamba ”Wema ni mtoto hakui, yani miaka inakwenda bado yuko vile vile”, amesema Martin Kadinda.

Martin ameendelea kwa kusema kwamba …”Wema ana maisha yake binafsi, ana vitu vyake anavyovipenda kwa hiyo ninachokifanya zaidi ni kuweza dhibiti mambo yake binafsi yasimfanye kesho na kesho kutwa kushindwa kupata ugali wake wa kila siku”.

Kwa sasa Martin Kadinda amesimama kumsimamia msanii huyo kutokana na kubanwa na masomo, huku akisema kwake atabaki kuwa msimamizi wa msanii huyo pale panapohitajika mchango wake.

Martin Kadinda ameyasema hayo alipokuwa akihojiwa katika kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio.

 

Video: Tamko la Kenyatta kuhusu maandamano ya NASA
LeBron James: Sitakubali Trump kutumia michezo kutugawanya