Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi Simba SC, Mwina Kaduguda ‘Simba wa Yuda’ amehoji maamuzi ya Uongozi wa klabu hiyo kumfuta kazi Kocha Franco Pablo Martin.

Simba SC leo Jumanne (Mei 31) imetangaza rasmi kuachana na Kocha Pablo, kwa makubaliano ya kuvunja mkataba yaliofanywa na pande zote mbili.

Kaduguda ambaye hakuwa sehemu ya viongozi waliokwenda Mwanza kushuhudia mchezo wa Nusu Fainali Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ dhidi ya Young Africans, amesema haoni sababu ya kocha Pablo kuondolewa.

Amesema Kocha huyo aliikuta Simba SC imeshafanya usajili na baadhi ya mambo mengine ya kiufundi, hivyo hakupaswa kufukuzwa kwa kigezo cha kushindwa msimu huu.

“Makocha wamekuwa wakitimuliwa bila sababu, mfano Pablo kafika katikati ya msimu timu kasajiliwa, anatimuliwa kwa kosa lipi? Je, kwenye makubaliano yake alivyokuwa anavihitaji mmemtekelezea?” amehoji Kaduguda

Bombadier yapata ajali Kigoma
Franco Pablo afungasha virago Simba SC