David Kafulila, aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Kigoma Kusini ameianza vizuri kesi aliyoiwasilisha katika Mahakama Kuu ya Kanda ya Tabora kupinga ushindi wa mgombea wa CCM, Husna Mwilima.

Mahakama hiyo jana ilitupilia mbali pingamizi lililowasilishwa mahakamani hapo na wakili wa Mwilima akiiomba Mahakama kutupilia mbali kesi ya msingi iliyofunguliwa na Kafulila kwa madai kuwa haikufuata utaratibu sahihi.

Jaji Leila Mgonya alitoa uamuzi wa kuruhusu kesi ya msingi kuanza kusilizwa kama ilivyowasilishwa mahakamani hapo.

Aidha, Mawakili wa Kafulila, Tundu Lissu na na Daniel Lumenyela wameiomba mahakama kuamuru mteja wao alipwe gharama zilizotokana na pingamizi lililowekwa walilodai lina nia ya kupoteza muda na kuweka usubumbufu.

Kesi hiyo inaendelea leo kwa kutathmini kiasi cha fedha ambacho mlalamikaji anapaswa kulipa kama dhamana ya kesi ili kesi ya msingi ianze kusikilizwa.

Dk Slaa Amzungumzia Rais Magufuli, Amshauri
Aliyekuwa Bosi wa TRA anaswa ufisadi wa Mabilioni, Magufuli Ashusha Rungu