Waziri wa kilimo Japhet Ngailonga Hasunga, amesema kuwa uzalishaji wa zao la kahawa umeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka uliopita .
Akizungumza na wazalishaji wa zao hilo mkoani Kagera, amesema kuwa kutokana na mfumo wa kutoa malipo ya awali kwa wakulima, uzalishaji kahawa ya maganda unatarajiwa kufikia kilo milioni 70, na kahawa safi kufikia kilo milioni 30.
“Kutokana na uzalishaji ambao umekuwa mzuri kwa mwaka huu, mkoa wa Kagera pekee yake mpaka sasa hivi kahawa ambayo imekusanywa kutoka kwa wakulima ni kilo milioni 64 , na matarajio yetu ni kukusanya kilo milioni 75 za kahawa ya maganda, na ikishabanguliwa tunapata kahawa safi na matarajio yetu ni tani elfu 35 ” amesema Hasunga.
Waziri Hasunga amesema kuwa kahawa iliyokusanywa mpaka hivi sasa ina thamani ya bilioni 76.8, ambazo ndiyo fedha zinazokwenda kwa wakulima baada ya makato kwenye halmashauri .
bofya hapa…..