Waziri wa kilimo Japhet Ngailonga Hasunga, amesema kuwa uzalishaji wa zao la kahawa  umeongezeka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na mwaka uliopita .

Akizungumza na wazalishaji wa zao hilo mkoani Kagera, amesema kuwa kutokana na mfumo wa kutoa malipo ya awali kwa wakulima, uzalishaji  kahawa ya maganda  unatarajiwa kufikia kilo  milioni 70, na kahawa safi kufikia kilo  milioni 30.

“Kutokana na uzalishaji ambao umekuwa mzuri kwa mwaka huu, mkoa wa Kagera pekee yake mpaka sasa hivi kahawa ambayo imekusanywa kutoka kwa wakulima  ni kilo milioni 64 , na matarajio yetu ni kukusanya kilo milioni 75 za kahawa ya maganda, na ikishabanguliwa tunapata kahawa safi na matarajio yetu ni tani elfu 35  ” amesema Hasunga.

Waziri Hasunga amesema kuwa kahawa iliyokusanywa mpaka hivi sasa ina thamani ya bilioni 76.8, ambazo ndiyo fedha zinazokwenda kwa wakulima baada ya makato kwenye halmashauri .

bofya hapa…..

Waandamana uchaguzi kucheleweshwa
Tanzania yapaa kwa ubunifu