Timu ya Kagera Sugar imedhamiria kumaliza Ligi Kuu msimu huu 2021/22 kwa kishindo, huku akijipanga kukusanya alama 12 za michezo minne iliyosalia.
Kagera Sugar itacheza nyumbani mwanzoni mwa juma lijalo dhidi ya Biashara United Mara ilinayopambana kujinusuru kushuka daraja, baada ya kufanya vibaya katika michezo kadhaa iliyopita.
Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar Buberwa Bilikes amesema, tayari kikosi chao kimeshaanza maandalizi ya kuelekea mchezo ujao, na wamejipanga kushinda ili kufanikisha mpango wa kukusanya alama 12 katika michezo minne iliyosalia.
Amesema mchezo dhidi ya Biashara United Mara utakua na vuta ni kuvute, lakini maandalizi wanayoyafanya hivi sasa, wana uhakika wa kuanza kukusanya alama tatu na zingine tisa zitafuata.
“Kikosi kimerudi mazoezini baada ya mapumziko ya siku chache, wachezaji wote wapo katika hali nzuri, tunajiandaa na mchezo wetu dhidi Biashara United Mara ambao tunaamini utakua mgumu, ila tutapambana ili tupate alama tatu muhimu,”
“Tuimedhamiria kumaliza msimu kwa kishindo kikubwa, tumepanga kuzipata alama zote 12 za michezo minne, tutaanza na mchezo wetu dhidi ya Biashara United, wachezaji tumeshaambia hili na watatekeleza kwa kupambana uwanjani.” Amesema Buberwa
Kagera Sugar imejipanga kumaliza katika nafasi nne za juu msimu huu, na hadi sasa ipo nafasi nane ikiwa na alama 33 zilizopatikana katika michezo 26 waliocheza.